Rinaldo wa Nocera

Rinaldo wa Nocera, O.S.B.Cam. (1150 hivi - 9 Februari 1217) alikuwa askofu wa Nocera Umbra, Umbria, Italia) tangu mwaka 1213 hadi kifo cheke.

Mtoto wa familia tajiri, akiwa kijana aliacha mali yake yote akawa mkaapweke hadi alipojiunga na Wabenedikto Wakamaldoli.

Baada ya kuteuliwa kuwa askofu aliendelea kushika sawasawa maisha ya kimonaki akawa rafiki wa Fransisko wa Asizi[1].

Tangu kale huheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Februari[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/40200
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy